Bajeti ya kitaifa kuwasilishwa Bungeni
Wednesday, 10 June, 2026
Waziri wa Fedha, Mheshimiwa John Mbadi, anatarajiwa kuwasilisha na kusoma Bajeti ya Kitaifa ya mwaka wa kifedha wa 2026/2027 mbele ya kikao cha Wabunge siku ya Alhamisi, tarehe 11 mwezi huu.
Bajeti hii ya trillioni Kshs 4.8 inaangazia kwa karibu mpangilio wa kiuchumi wa Rais William Ruto.
Kusomwa kwa Bajeti ya Taifa kutawezesha Wakenya kuelewa mipangilio ya kifedha na mipango maalum itakayo peana mwelekeo wa kiuchumi wa taifa kwa mwaka ujao.
#BudgetKE2026