Mswada wa Watoa Huduma za Rasilmali Pepe wa 2025 (Virtual Assets Service Providers Bill, 2025)
Tuesday, 3 June, 2025
Mswada wa Watoa Huduma za Rasilmali Pepe wa 2025 (Virtual Assets Service Providers Bill, 2025)๐๐ญ๐๐ง๐ ๐ฎ๐ฅ๐ข๐ณ๐ข
Mswada wa Watoa Huduma za Rasilmali Pepe Mali (Mswada wa Bunge la Taifa Nambari 15 wa 2025) ni Mswada unaodhaminiwa na Kiongozi wa walio Wengi Bungeni.
Mswada ulichapishwa tarehe 17 Machi 2025. Ulisomwa kwa mara ya kwanza tarehe 8 Aprili 2025.
Baada ya hapo, Kamati ya Fedha na Mipango ya Taifa ilikabidhiwa Mswada.
๐๐ฌ๐ก๐ข๐ซ๐ข๐ค๐ข๐ฌ๐ก๐ฐ๐๐ฃ๐ข ๐ฐ๐ ๐๐ฆ๐ฆ๐
Kamati inatakiwa kuuzingatia Mswada, kualika maoni kutoka kwa umma, na kuandaa ripoti yake na mapendekezo ya marekebisho yoyote inayoona yanafaa.
Katiba inatambua umuhimu wa kushirikisha umma katika kutoa maoni kuhusu masuala ambayo yanawaathiri. Hivyo, *Ibara ya 118(1) (b) ya Katiba ya Kenya* inaelekeza kwamba Bunge lazima iwezeshe ushirikishwaji wa umma na umma lazima ipewe fursa ya kutoa maoni kwenye Mswada kama huu.
Ushirikishwaji wa umma (public participation) ni agizo la kikatiba. Wananchi wako huru kutoa maoni yao kuhusu Mswada huu na wanaweza kuunga mkono Mswada au kupinga Mswada. La muhimu ni kutoa sababu ili Kamati ya Kiidara ya Fedha na Mipango ya Taifa ishughulikie kwa kina maoni yako.
Shughuli hii ya vikao vya umma vitaanza leo ๐๐ฎ๐ฆ๐๐ง๐ง๐ ๐ญ๐๐ซ๐๐ก๐ ๐ ๐๐ฎ๐ง๐ข ๐ก๐๐๐ข ๐๐ฃ๐ฎ๐ฆ๐๐ ๐ญ๐๐ซ๐๐ก๐ ๐ ๐๐ฎ๐ง๐ข, ๐๐๐๐ katika Kaunti zifuatazo: ๐๐ข๐ ๐จ๐ซ๐ข, ๐๐ฎ๐ฌ๐ข๐, ๐๐๐ง๐๐ข, ๐๐ซ๐๐ง๐ฌ ๐๐ณ๐จ๐ข๐, ๐๐๐๐ก๐๐ค๐จ๐ฌ, ๐๐ข๐๐ฆ๐๐ฎ, ๐๐จ๐ฆ๐๐๐ฌ๐, ๐๐ฐ๐๐ฅ๐ ๐ง๐ ๐๐ข๐ฅ๐ข๐๐ข.
๐๐ฎ๐ก๐ฎ๐ฌ๐ฎ ๐๐ฌ๐ฐ๐๐๐
Lengo kuu la Mswada ni kutoa mfumo wa kisheria wa kusimamia watoa huduma za rasilmali pepe.
Mswada unaangazia hatari zinazoweza kutokea kutokana na matumizi mabaya ya bidhaa na huduma za rasilmali pepe.
Hivyo basi, Mswada unaainisha *Mamlaka ya Masoko ya Mitaji (Capital Markets Authority)* na *Benki Kuu ya Kenya (Central Bank of Kenya)* kama mamlaka kuu za udhibiti wa huduma za rasilmali pepe na watoa huduma za rasilmali pepe.
Kazi za jumla za mamlaka za udhibiti zilizoteuliwa zimetolewa chini ya kifungu cha 7 cha Mswada kujumuisha:
โข kutoa leseni kwa watoa huduma za rasilmali pepe
โข kusimamia, kusimamia na kufuatilia watoa huduma za rasilmali pepe
โข kutoa maelekezo, maagizo na kuchukua hatua za utekelezaji, kama inavyoonekana ni muhimu
โข kutoa na kuchapisha matangazo, miongozo, vidokezo vya mwongozo na vyombo vingine
Kwa mujibu wa Mswada, itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kufanya biashara ya huduma za rasilmali pepe bila kupata leseni kutoka kwa mamlaka husika.
Mswada unaelekeza kwamba mtu yeyote anayetafuta kufanya biashara ya mtoa huduma za rasilmali pepe atawasilisha maombi ya leseni kwa mamlaka husika ya udhibiti kwa kufuata mahitaji kama inavyoweza kuwekwa na kuambatana na ada iliyowekwa ya maombi.
๐๐ข๐ญ๐ข๐ฆ๐ข๐ฌ๐ก๐จ
Vikao hivi vya umma vinatoa fursa nzuri kwa wananchi na wadau wote kutoa maoni yao kwenye Mswada huu. Mswada huu bado haujakuwa sheria. Baada ya maoni yote kukusanywa, Kamati itaketi kisha izangatie maoni yenu na kutoa ripoti ambayo itawasilishwa katika Bunge la Taifa. Baadaye, mswada huu utafanyiwa marekebisho kabla kupitishwa kuwa sheria.